💞MPE MKEO VITU HIVI ATAFARIJIKA💞
Amani ya Moyo Wa Mwanamke ni Kitu Cha Thamani Mno Katika Maisha ya Mwili wake na Akili yake na Piah ni Kitu Pekee na Zawadi ya Hali ya Juu inayompa Faraja na Kumdhihirishia Ishara Ya Upendo,Mahabbah,Hubba na Kuthaminiwa.
Na Wala Haridhishwi na Kero,,Ubabe,Kufokewa kila Wakati na Kudharauliwa Mara Kwa Mara na Kuonekana Kuwa Nafasi ya Thamani yake Kwa Mume Wake ni ya Hadhi ya Nyama ya Nguruwe.
Hadhi Ambayo,,Isiyoguswa,Isiyonuswa,Isiyosogelewa wala Isiyoshikiliwa Kutokana na Uchafu wake na Unajsi wake. #usiwe_hivyo_ndugu_yangu.
Kila Unapomuumiza Mkeo Katika Hisia Zake,,Basi Hupururuka Amani ya Moyo Wake.
MFANYIE HAYA MKEO KUANZIA LEO.
1).TENGA MUDA WA KUKAA NAE.💞
Kama haukuwa na Utaratibu wa Kuketi Sehemu tulivu na Mkeo Mkazungumza Yaliyo ndani ya Mioyo yenu kabla Hata ya Kulala kwenu. Basi Jua Umeshautia Madoa Moyo Wake na Kuzikwaruza Hisia Zake.
Tenga,,Muda wa Kukaa na Mkeo Hata Kwa Dk10,,Ukisikilize Alichonacho nawe Umpe Ukichonacho.
2).KILAINISHE KINYWA CHAKO JUU YAKE.🌹
Kuwa na Maneno Matamu na Lainiii,,yaliyojawa Mahabbah na Hubba la Mazungumzo na Yenye Upole wa Mawimbi Kila Mara Uzungumzapo na Mke Wako.
Kamwe Usiwe ni Wa Kufoka foka Juu yake,,,Hata Akikukosea Mweleze Makosa Yake kwa Upole na Mahabbah ya Hali ya Juu, Atakuelewa Wala Hatokupuuza,,na Utafurahika Moyo wake na Hatokuchoka Ndani ya Moyo wake. #lugaha_tamu yenye Upole Inaeleweka Mno kwa Mke Wako #kuliko_kufoka_kwako.
3)KUWA RAFIKI KWAKE NA MSAIDIZI WAKE💕.
Mapambano Ya Furaha Ya Moyo wa Mkeo Hayatofanikiwa Ispokuwa Kwa Weredi Wako wa Kushiriki kwako.
Juwa Kuwa,,Mkeo nae Ni Mwanadamu,Huwa Anachoka na Anahitaji Mapumziko,,Jitahidi kwa Kadri ya Uwezo wako Kumsaidia Mke Baadhi ya Shughuli za Ndani Kwako.
Hata Kama Huwa Hazimchoshi wala Kumuumiza; Lakini Jua Kumsaidia kwako Kutazigusa Hisia Zake na Kuyanyanyua Mapenzi yake. Cheka nae Taniana nae Mpe kila Anachostahili. #huyo_ni_mkeo
4).JIWEKE KARIBU NA MWILI WAKE.💞
Mume juwa Kuwa "Wewe ni Vazi kwa Mkeo naye ni Vazi kwako Wewe"
Iwekee Mikono yako Urafiki wa Karibu na Mwili wa Mke Wako
Mkumbatie Mkeo Kila Uingiapo Ndani Kwako,Na Usiiweke Mbali na Mwili Wake Pale Mzungumzapo,na Kijaalie Kichwa Chake Kuwa ni Halali ya Kifua Chako,Kuwa Msaidizi Wa Kuusafisha Mwili wake Pale Muogapo na Kumpaka Mafuta yake kwa Mikono yako na Usiache Kumvalisha Mavazi yake #pale_mmalizapo.
#ndoa_ni_tamu TUSIO NDOANI TUFANYE HIMA.

Mama Michongo
Delete Comment
Are you sure that you want to delete this comment ?
Milliam Tz
Huwezi Kuwa na thamani kwa kila mtu, Huwezi kuhurumiwa na kila mtu Na pia kamwe huwezi kukubalika na kila mtu.
Ukifahamu haya Itakusaidia kutokuumiza kichwa pale utakapoona kuna watu hawakuthamini, hawakuonei huruma wala kukukubali maana mambo hayo yote ni kawaida kwa mwanadamu kutokea.
Delete Comment
Are you sure that you want to delete this comment ?
IGIRANEZA468 Innocent
Delete Comment
Are you sure that you want to delete this comment ?